Grumeti Fund 2019 Swahili Impact Report
Ili kuleta mabadiliko ya haraka, serikali, makampuni binafsi, jamii na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) hawana budi kuboresha jinsi wanavyofanya kazi na kushirikiana. Kubadilishana maarifa ni kiungo muhimu katika kuleta mabadiliko haya. Mashirika yenye uzoefu wa muda mrefu kama Grumeti Fund yana jukumu la kushiriki katika kutafuta na kutoa ufumbuzi juu ya changamoto za kiuhifadhi na maendeleo ya jamii.